Psalms 57:7-11


7 aEe Mungu, moyo wangu ni thabiti;
nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

8 bAmka, nafsi yangu!
Amka, kinubi na zeze!
Nitayaamsha mapambazuko.


9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;
nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

10 cKwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni,
uaminifu wako unazifikia anga.


11 dEe Mungu, utukuzwe juu mbinguni,
utukufu wako na uwe duniani pote.
Copyright information for SwhKC